Staa wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’.
Staa wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amedaiwa kujiweka kwa
Pedeshee Chifu Kiumbe baada ya siku kadhaa zilizopita kumfuata na
kumtaka amsaidie katika project ya filamu yake .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya msanii
huyo kupewa sapoti ikiwa ni pamoja na gari la kushutia, mdada huyo
amekuwa akijionesha kuwa pedeshee huyo ni mtu wake.
“Alipopewa sapoti hiyo akaona ndiyo ajiweke kabisa bila kujua kuwa
Chifu Kiumbe alikuwa akimsaidia tu na wala hakuwa na wazo la kumtaka,”
alidai sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Pedeshee Chifu Kiumbe.
Baada ya habari hizi kunaswa, mapaparazi wetu walimtafuta pedeshehe
huyo ambaye alisema: “Hata mimi nashangaa kusikia watu wakisema natoka
na yule dada, ukweli sijawahi kuwa mpenzi wake alikuja kuniomba msaada
wa project yake nikamsaidia hata gari nilimpatia lakini nimesikia eti
ananiita bebi kwenye mitandao ya kijamii, siyo kweli kabisa.”
Batuli.
Batuli naye anasemaje? Huyu hapa: “Mh! Watu wananisema mengi sana,
waache waseme, mimi naongea na Chifu kawaida tu, hata jana nilimfuata
anisaidie kama wasanii wengine.”
0 comments:
Post a Comment