STEVE NYERERE NA SANDRA WAGANDANA KAMA RUBA

MAHABA? Prezidaa wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na mwigizaji mwenzake, Salama Salmin ‘Sandra’ wamezua minong’ono kufuatia kitendo chao cha kugandana kama ruba ukumbini.
Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye uzinduzi wa filamu tatu za Kiswahili ‘Swahiliwood’ kwenye Ukumbi wa Century Cinemax, Oysterbay jijini Dar wikiendi iliyopita.
Katika tukio hilo, wakiwa ukumbini hapo wawili hao karibu muda wote walionekana wakipozi kimalavidavi  huku Steve Nyerere akikumbatia ‘pimajoto’ la mwanadada huyo, ishu iliyosababisha wapiga chabo kuanza kuwajadili.
Hawakuishia hapo kwani wakati wa vitafunwa, wawili hao walionekana ‘wakishea’ kwenye sahani moja huku shosti mmoja wa Sandra akiwafuata kwa nyuma na kuwamwagia sifa kwa namna walivyopendeza.
Kufuatia tukio hilo, ‘kachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) alianza kuwafuatilia na kuwafotoa picha kadhaa lakini wawili hao walionekana kutojali na wakati mwingine waliweka pozi tata.
Juhudi za OFM kupata undani juu ya ukaribu wa mastaa hao ziligonga mwamba baada ya kutaka waachwe wapumzike.
Katika hafla hiyo, filamu zilizozinduliwa ni Network, Mdundiko na Sunshine chini ya Kampuni ya Pron Promotions Production huku shughuli hiyo ikuhudhuriwa na mastaa kibao wa Kibongo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini