
Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray’ katika pozi.
WAPENDANAO,
Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray’ waligeuka mapedeshee kwa muda baada
ya kummwagia fedha za kutosha, Mkuruguenzi wa Bendi ya Extra Bongo,
Ally Choky.
Tukio hilo lililoteka hisia za mashabiki wa bendi hiyo lilitokea
juzikati katika Ukumbi wa Meeda, Dar ambapo Ray aliyekuwa ameambatana na
ubavu wake huo, walionekana ukumbini humo wakipata vinywaji, baadaye
muda ulivyozidi kwenda, wakanogewa na rhumba la Choky na kuanza kutunza.
“Mh! Leo mtu na mtuwe wamegeuka mapedeshee, wanamwaga minoti ya kufa
mtu, hata hazihesabiki…hatari,” alisikika shabiki mmoja aliyeshuhudia
tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment