Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli amesafiri akitokea Mkoani Dodoma anakohudhuria Vikao vya Bunge la Katiba na kwenda moja kwa moja Morogoro maeneo ya Mikese (Kilomita kumi kutoka Mzani wa Mikese kuelekea Dar), ambapo magari mawili yaligongana na kuteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtu mmoja alietambulika kwa jina la Moud Amin.
Ajali
hiyo ambayo imetokea mapema leo ilifunga barabara yote ya Dar -
Morogoro, takribani kwa masaa zaidi ya mawili na kusababisha foleni
kubwa ya takribani kilomita 30. Malori hayo, lori moja lilikuwa
likitokea Bukoba, mkoani Kagera likielekea Dar na lori lingine
likielekea Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Aidha,
Dkt. Magufuli kwa mamlaka aliyopewa, ameruhusu malori yaliyokuwa
yamesongamana kupita mzani wa Mikese bila kupimwa ili kuondoa usumbufu
mwingine katika mzani wa Mikese.
Dkt. Magufuli kwa pamoja na mhandisi wa mkoa wa Morogoro Mhandisi Tenga walisimamia ukwamuaji wa malori hayo.

Dkt. Magufuli akiongea na baadhi ya wahanga wa ajali hiyo.

0 comments:
Post a Comment