Msanii
nyota kwenye tasnia ya filamu za kibongo Jacqkline Wolper na Manaiki
Sanga, anayejulikana kama The Don, wako katika bifu kubwa kisa kikiwa ni
picha walizopiga pamoja.
Tukio
hilo limechukua sura mpya kwenye mitandao ya kijamii baada ya wiki
mbili zilizopita gazeti hili kuanika picha za mastaa kadhaa waliowahi
kupiga picha zilizozua minong’ono mitaani, kutokana na tabia ya Manaiki
kuaminika kuwa ni wanawake aliotembea nao.
Maskani Bongo liliandika juu ya Wema Sepetu kunasa kwenye mtandao wa ngono, huku likionesha picha yake kubwa akiwa na Manaiki Sanga wakiwa wamekumbatiana huku picha ndogo ndogo za wasanii wengine maarufu akiwemo Jackline Wolper nao zikiwaonyesha wakiwa na mcheza filamu huyo.

Baada ya
habari hiyo kutoka, baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo walichukua
kurasa za gazeti hilo na kuiweka mtandaoni na watu walipoanza kutoa
maoni yao, Jack alimzungumzia Manaiki na kukanusha kuwahi kushiriki naye
mapenzi.Mjadala mkali ulizuka huku mashabiki wa wasanii hao
wakisemana vikali ambapo Wolper aliomba kuelezea jinsi ilivyokuwa hadi
akakutana na Manaiki, akasema “Duh yaani mimi nimekuwa mpenzi wa Manaiki
tena? Huyu mshikaji alishaahidi kuwa kwa gharama yoyote atakuwa staa,
hivyo akatoa mkwanja wake watu tukaula basi,” alisema Wolper.
0 comments:
Post a Comment