HUYU NDIYE MZUNGU ALIYEKAMATWA NA KILO 5 ZA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR-ES-SALAAM


Raia wa Henellic, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.

Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini  Zurich, Uswisi.
Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.
Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo  akisubiri taratibu za kisheria ili afunguliwe mashtaka.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini