AUNT EZEKIEL AANGUKA KWA PRESHA...ALAZWA HOSPITALINI

Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel.

STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuanguka ghafla kwa presha akiwa ‘location’ jijini Tanga, Risasi Jumamosi lina habari hii.
Kwa mujibu wa chanzo, Aunt  akiwa katika harakati za kuigiza filamu anayocheza na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, ghafla alianguka na kukimbizwa katika Hospitali ya Gesha jijini humo.

 
Aunt Ezekiel akiwa hospitali amelazwa.
Baada ya kuzipata habari hizi, mapaparazi wetu walimtafuta Aunt kwa njia ya simu  na alipopatikana alikiri kuanguka kutokana na kusumbuliwa na presha ya kushuka.
 “Kweli  nilikuwa shutting na Mzee Majuto, ghafla nilianguka na kukimbizwa hospitali, wameniwekea dripu mkononi ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri,” alisema Aunt.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini