WAKATI MGOMO WA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA UKIINGIA SIKU YA TATU LEO, TRA YASEMA HAITATUMIA UBABE TENA KUYAFUNGA MADUKA YA WASIO NA MASHINE ZA EFD



Wakati mgomo wa wafanyabiashara mkoani Mwanza unaendelea, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haitatumia ubabe kuwafungia maduka ambao watashindwa kuwa na Mashine za Kielektroniki (EFD). 
 
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema wameweka mikakati ya kuwaelimisha wafanyabiashara.
 
Miongoni mwa mikakati hiyo, ni kuwatembelea na kuwashauri, kuwakumbusha na kuwatoza faini ya asilimia tano hadi kumi kwa ambaye hajatekeleza utaratibu wa kutumia mashine hizo.
 
Wakati TRA wakisema hayo, polisi mkoani Mwanza jana walipita mitaani kuwataka wafanyabiashara kufungua maduka bila mafanikio.
 
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, alidai kuwa mgomo wao waliouanza tangu juzi utaendelea.
 
Sanjari na mgomo huo kuendelea, Taasisi ya Sayansi ya Jamii (Tasaja) imeitaka Serikali kuwasikiliza wafanyabiashara kwa vile madai yao yana msingi.
 
Taasisi hiyo iliishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuzitoa mashine hizo bure, ili kuepuka migogoro katika utekelezaji mkakati huo wa kuweka mpango mzuri wa ukusanyaji kodi.
Ofisa Habari wa Tasaja, Bituro Kazeri alisema licha ya kutokukubaliana na mgomo wa wafanyabiashara, hoja yao ina msingi.
 
Kazeri alisema gharama za mwanzo za kununua mashine hizo siyo jukumu linalopaswa kubebwa na mfanyabiashara pekee, bali kwa ushirikiano na Serikali.
 
Mgomo wa wafanyabiashara wa maduka makubwa na madogo jijini hapa, jana uliingia siku ya pili baada kususia kikao cha kutafuta mwafaka kilichokuwa kiendeshwe na ofisi ya mkuu wa mkoa.
 
Wakati mgomo huo ukiendelea, baadhi ya magari ya polisi yalionekana jana asubuhi yakizunguka mitaa mbalimbali.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini