RIYAMA
amesema kuwa anachukizwa na vitendo vya kimapenzi vinavyoonyeshwa
kwenye filamu nyingi za sasa, ikiwemo mabusu ya staili ya kulana denda.
Riyama
alisema kuwa zamani walikuwa wanapigana mabusu mashavuni kama ishara ya
mapenzi na kusameheana, lakini sasa wanakula denda kabisa.
“Vitendo
hivi ni uchafu wa wazi kwenye jamii, hata kama kuna namna ambavyo
wanafanya lakini bado kuna tatizo, mtazamaji ambaye ni mtoto, kijana,
mzee haelewi hilo, yeye anajua wanapeana denda kitendo hiki sikipendi,”
alisema.
Riyama
aliwajia juu wale wote wanaopenda kuigiza uzungu uliopitiliza kwa kuwa
imekuwa ikizua lawama miongoni mwa wadau wa filamu.
“Hii
ni ajira yetu, ni heshima kwa familia zetu, bado tuna nafasi ya
kuifanya iwe bora na ya kuheshimika kuliko kuiga vitu ambavyo vinafanya
ionekane katika mtizamo usio wa kiungwana wakati waigizaji ni waungwana
kama watu wengine lakini matendo ndiyo yanayotuangusha,”alisema.
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa filamu zinazoigizwa nchini kuhusisha vitendo vya aina hiyo licha ya baadhi ya watu kulalamika.