Picha za Bi Harusi mtarajiwa ambaye ni modal sexy Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ hivi karibuni zimenaswa akiwa katika mapozi ya kimahaba na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Martin.
Picha hizo ambazo zipo kwenye mtandao zinawaonesha wawili hao wakijiachia kwenye Ufukwe wa Mbalamwezi uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, mazingira yaliyosababisha baadhi ya watu kuhoji juu ya ukaribu wao huo
Katika kujua uhusiano uliopo kati ya wawili hao, mpekuzi wetu alimtafuta Jack kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kupatikana mara moja.