
Mwanamuziki Chipukizi kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Abdallah Ramadhani Manyuti "D-Manyuti"
anaetamba na wimbo wake mpya wa "Tamtam" amesema fikra zake kwa sasa ni
za kimataifa na si Tanzania tena kwa vile amejipanga kufika huko hivyo
kwa uwezo wa Mungu atafika bila shaka.
Akiongea
na Xdeejayz mwanamuziki huyo alisema" Unajua maisha ni malengo hivyo
kila utakachokipanga kitakuwa hivyo kwa hiyo mimi nimepanga kuufikisha
muziki wangu kwenye levo ya dunia na naamini Mungu atanijalia hivyo"
Alisema mwanamuziki huyo

Aidha
D-Manyuti anashukuru kwa sasa amepata meneja wa kumsimamia kazi zake
ambae anaitwa Maneno ambae nia ndiye meneja burudani Club Jakalanda
hivyo anaamini kwa uzoefu mkubwa aliokuwa nao Maneno basi atamsaidia
kufanikisha ndoto zake .
Wimbo huo amemshirikisha mwanadada Missyuna na umekuwa wimbo unaoongzwa kupigwa sana kwenye vituo vya redio nchini.
Wimbo huo amemshirikisha mwanadada Missyuna na umekuwa wimbo unaoongzwa kupigwa sana kwenye vituo vya redio nchini.