
SURA
ya mauzo katika sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’
ametoa ya moyoni kuwa kama siyo kuwekwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya
Segerea, Dar basi yangemkuta mazito.
Lulu
alikaa Gereza la Segerea kwa takribani miezi kumi baada ya kutokea kifo
cha aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’
aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.
Nyota huyo wa Filamu ya
Foolish Age alifunguka mambo ya kushangaza hivi karibuni juu ya tukio
hilo kupitia Kipindi cha Take-One, kinachorushwa na Clouds TV.
TATIZO FOOLISH AGE
Lulu
alikuwa akizungumzia filamu yake hiyo ya Foolish Age ambapo alisema
sinema hiyo inawasihi wasichana ambao wanapitia kipindi cha balehe
ambacho ni hatari sana kwao.
“Kwa kweli kipindi cha foolish age ni cha hatari sana, nilicheza filamu hiyo ili kuwaasa wasichana wenzangu.
“Asikwambie mtu, mimi mwenyewe nilikokuwa nikielekea si kuzuri kabisa.

“Ukweli
ni kwamba kama siyo matatizo (kifo cha Kanumba) nikaenda mahabusu sijui
ingekuwaje sasa hivi. Kukaa jela kulinisaidia kusitisha kasi ya tabia
yangu, nikatoka nikiwa mpya.
“Yangenikuta mazito zaidi maana kipindi kile ilikuwa hatari tupu,” alisema Lulu ambaye ni mrembo wa haja.
Staa huyo aliongeza kuwa kipindi hicho kilikuwa cha hatari na hakitamani kijirudie hata kidogo katika maisha yake.
Alisema
kwamba si ajabu inawezekana kipindi hicho ndicho kilisababisha matatizo
yote yaliyomkuta. Alisema alikuwa akielekea kubaya.
HATAKI KIJIRUDIE
“Ni
kipindi ambacho siwezi kukuhitaji tena katika maisha yangu si kizuri na
kinatisha maana kuna wakati nilikuwa sisikii la mtu yeyote hata mama
yangu mzazi,” alisema Lulu ambaye baada ya kutoka mahabusu haonekani
akirandaranda mjini kama zamani.
Kabla ya utulivu huo
alioupata nyuma ya nondo, Lulu alikuwa hakauki kwenye kumbi za usiku za
starehe huku akilewa tilalila na kuyaweka maisha yake hatarini endapo
angefanyiwa kitu mbaya.
Lulu alihusishwa na
kifo cha Kanumba kwa kuwa siku ya tukio alidaiwa kuwa naye eneo la tukio
ambapo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana akisubiri kesi ya
kuua bila kukusudia.

Wakati hayo hayajapoa kumeibuka skendo mpya inayomgusa staa huyo mkubwa Bongo.
Madai
mazito yameshushwa na wafuatiliaji wa mambo ya watu kuwa nyuma ya
mwanadada huyo anayeng’ara kuna mbunge maarufu anayemiliki jimbo kwa
kura za wananchi jijini Dar (tutamtaja baadaye).
ILIKUWA HIVI
Sosi: Hivi ninyi Global siku hizi hamuandiki skendo za mastaa?
Global: Tunaandika sana kwani vipi?
Sosi: Mna habari?
Global: Tunazo nyingi fuatilia magazeti yetu lakini ukitupatia ya kwako tutairusha hewani.
Sosi: Sasa mimi nina habari yangu.
Global: Inakuhusu wewe? Funguka.
Sosi: Hainihusu mimi. Ni ya ‘Kalulu Kadogo’.
Global: Siku hizi amekua, sema Lulu inatosha. Eeh... hiyo habari ikoje?
Sosi:
Kwa taarifa yenu siku hizi anatoka na mbunge (anamtaja). Ndiye
kamnunulia lile gari analokatiza nalo mjini na kampangishia bonge la
mjengo kule Tegeta (Dar). Fuatilieni kwa watu wake wa karibu, naombeni
msinitaje.
Global: Hatuwezi kukutaja ngoja tuzame mzigoni.
Gazeti
hili lilifanya uchunguzi wake kwa watu wa karibu wa Lulu na kubaini
kuwa ni kweli kwa sasa staa huyo amehama Tabata alikokuwa akiishi na
mama yake, Lucresia Karugila na kuhamia kwenye bonge la mjengo Tegeta
huku akisukuma gari kali (aina haikujulikana mara moja).
Madai mengine yalisema kwamba mke wa mbunge huyo alishamtafuta Lulu na kumuonya kuachana na mume wake.

Baada
ya kujiridhisha kuwepo madai hayo, juzi gazeti hili lilimtafuta Lulu na
kumsomea mashitaka yake mwanzo hadi mwisho ambapo alifyatuka:
“Hivi ni nani anayeleta habari zangu Global? Analipwa na nani? Maana kila kukicha unasikia hili, halijapoa unasikia lingine.
“Si
kweli kwamba natembea na huyo mbunge. Kwanza sina mazoea naye.
Nakumbuka nilimuona mara moja tu sikumbuki ilikuwa kwenye shughuli gani.
“Huyo mkewe mimi simjui anafananaje. Nasema huko ni kuchafuana kusikokuwa na maana.”
VIPI KUHUSU KUPANGISHIWA NYUMBA?
“Ni
kweli nimehamia Tegeta lakini sijapangishiwa, nimepanga mwenyewe. Hivi
nikifanya jambo lazima iwe kuna mwanaume? Watu waache hizo. Wabadilike.”
VIPI KUHUSU GARI?
“Gari ninalo muda mrefu nimenunua kwa fedha yangu. Halina mkono wa mbunge, ni jasho langu.”
Kabla
ya kuwekwa mahabusu, Lulu aliwahi kudaiwa kuhongwa nyumba na mbunge
mwenye kitambi kikubwa, ishu hiyo aliikanusha kwa nguvu zote.
Credit:GPL