Mwenyekiti
wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Wilaya ya Ilala, Michael Loswe
(kushoto), akisoma risala kwa mgeni rasmi, Edward Lowassa.
Mbunge
wa Jimbo la Segerea, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya
Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, akiongea na waendesha bodaboda (hawapo
pichani).
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa, leo asubuhi amewataka
waendesha pikipiki (bodaboda) wa wilaya zote za jijini Dar es Salaam
ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni kununua pikipiki zao badala ya
kuendelea kutumia pikipiki zinazowatajirisha watu wengine ambao
wanazimiliki.
Lowasa ambaye ni Mbunge wa Monduli aliwataka waendesha bodaboda hao
kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa (Saccos) ambazo zitawasaidia
kujiongezea kipato na kujinunulia pikipiki zao na kuachana na kuendesha
pikipiki za matajiri.











0 comments:
Post a Comment