
Alitua ghafla na kwenda kumuaga Mandela
*Aondoka
bila kumpa mkono wa pole Rais Zuma KATIKA
hali isiyotarajiwa, Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumatano iliyopita aliwashangaza
wengi baada ya kufika ghafla jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuaga mwili Mzee
Nelson Mandela na kuondoka mara moja.

Pamoja na kuwasili ghafla bila taarifa Pretoria, Kagame alikwenda moja kwa moja katika majengo ya Union Buildings na kwenda kuaga mwili huo kisha alielekea uwanja wa ndege na kuondoka.
Habari ambazo Rai Jumatano imethibitisha zinasema aliondoka saa chache baada ya kuuaga mwili wa shujaa Mandela na kuelekea Rwanda ambako alikwenda kuongoza Mkutano Mkuu wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF), ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.