Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’.
UAMUZI
wa kujitosa kuwania nafasi ya uenyekiti wa kundi la mastaa la Bongo
Muvi kwa mwigizaji Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, umempa wakati mgumu
mwenyekiti anayemaliza muda wake wa kuliongoza kundi hilo, Vincent
Kigosi ‘Ray’ kwa hofu ya kuidondosha nafasi hiyo tamu.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki
iliyopita kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa wasanii wakubwa
wa kundi hilo alisema tangu Dk. Cheni atangaze nia ya kuwania nafasi
hiyo, Ray amekosa raha kutokana na ubora wa sera ambazo Dk. Cheni
amekuwa akizinadi kwa wapiga kura.
“Ni kweli nagombea lakini si kwa ajili ya kumkomoa mtu, kiongozi
atachaguliwa kwa kuchuja ubora wa sera zake, hayo wanayosema kuwa
nitampindua kutokana na sera zangu, wana haki ya kusema,” alisema Dk.
Cheni.
-gpl
-gpl