GAUNI alilovaa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael hivi karibuni alipokuwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu limeonesha kuwatega wanaume hasa wakware kufuatia kuuanika ‘upaja’ wake.
Akiwa ndani ya Ukumbi uliopo ndani ya Hoteli ya Serena, Posta jijini
Dar, Lulu alionekana amevalia gauni refu lakini pembeni likiwa na mpasuo
mkubwa ambapo kila alipokaa, mapaja yake yalionekana wazi hivyo
kumfanya ahangaike kuyaficha huku wanaume nao wakitumia muda mwingi
kumkodolea macho kisha kunong’ona.
“Duh!Haka kabinti kazuri na lile gauni alilovaa ndiyo anawaacha hoi
sana wanaume,ile ni kututafuta ubaya na kama ni kututega kafanikiwa kwa
silimia 100,” alisikika kijana mmoja akisema.
Mwandishi wetu alifanya
jitihada za kutaka kuongea na Lulu juu ya mpasuo huo, lakini hakuwa
tayari na hata baada ya zoezi la utoaji wa tuzo, aliondoka fasta akiwa
na wapambe wake.
0 comments:
Post a Comment