MSANII wa filamu Bongo, Deogratius Shija amefunguka kuwa anatamani
sana kumuoa msanii mwenzake, Wastara Juma lakini anaamini kikwazo
kitakuwa ni dini.
Akistorisha na paparazzi wetu, Shija alisema tangu kabla msanii huyo
hajaolewa na aliyekuwa mumewe, Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, alikuwa
anampenda lakini bahati haikuwa yake hivyo kwa sasa anatamani ndoa na
mwanamke huyo.
“Unajua natamani sana kumuoa Wastara ila sidhani kama atakubali
kubadili dini kwani ni Muislamu haswa, kwa upande wangu siwezi kubadili
dini kwa sababu nampenda sana Yesu. Ila ni jambo linalozungumzika,”
alisema Shija.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Wastara ili kuzungumzia ndoto hiyo ya Shija lakini hakuweza kupatikana mara moja.
0 comments:
Post a Comment