Limegeuka kuwa jina lake na mwenyewe analitumia kikamilifu katika harakati za kimjini. Lakini aligeuka kuwa kipusa zaidi baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg mwaka jana, akiwa na shehena kubwa ambayo Tanzania ilijulikana kama madawa ya kulevya, lakini Afrika Kusini wakasema ni malighafi inayoweza kutumika kutengeneza mihadarati.
Sifa moja kubwa ya uzuri wa msichana huyu, ni maumbile yake ya nyuma, amejazia kiasi ambacho ni wanaume wachache, tena walio waadilifu kwelikweli, wanaoweza kupishana naye na wasigeuke nyuma kuhakikisha walichokiona!
Akiwa huko kwa Madiba, binti huyu alikuwa akiweka picha zake kila mara katika mitandao ya kijamii inayopatikana katika Internet, hasa Instagram. Ni utamaduni mpya kwa wasichana wa Kibongo siku hizi, wengi wanapenda kutupia picha zao humo na watu ambao huwaona, huwasifia kama wamependeza au huwaponda kama wamechukiza.
Lakini katika hali isiyotarajiwa kabisa, wiki kadhaa zilizopita, Masogange aliweka picha yake huko, ikionyesha sehemu kubwa ya mwili wake, ikiwa imepakwa hina.
Lakini kitu kibaya katika picha hiyo ni kwamba Masogange amepiga picha mguu wake akiwa amepaka hina hiyo hadi juu kabisa pajani.
Baadaye akapiga picha nyingine akiwa amevaa kimini, lakini kikionyesha sehemu ya paja hilo lililopakwa urembo huo ambao pia hutumiwa na wanawake wa Kiislamu wakati wa ndoa!
Ni picha ambayo mwanaume yeyote mkware akiiona, anavuta hisia za mahitaji ya kimapenzi. Na nieleweke, siyo Masogange tu anayetupia picha za aina hii, wasichana wengi hufanya hivi na baadhi yao, baada ya kuziweka, huweka pia na namba zao za simu, ukiwa na shida nao uwatafute!
Inakuaje mtoto wa kike, mwenye jina, tena na uzuri wako bomba kabisa wa asili, unapiga picha za namna ile na kuziweka hadharani? Nafikiri siyo sawa, zipo picha zinazopaswa kuendelea kubakia chumbani.
Kwa jinsi mambo yanavyotokea, unapata kabisa hisia kwamba kumbe dada zetu wanatafuta umaarufu kwa nguvu kwa malengo binafsi, yasiyo ya kimaadili na yenye kuchefua.
Wakishapata majina na bahati nzuri kuanza kufuatiliwa na vyombo vya habari, vikitanguliwa na magazeti, wanaanza makeke!
Kwa kutambua kwamba sura zao zinafahamika, badala ya kujistahi, ndiyo kwanza utashangaa kuona wanavaa mavazi yenye utata, kumbe tunaanza kuelewa kuwa wanafanya hivi ili kujitangaza, kama wanavyosema mabingwa wa uchumi, biashara matangazo.
Ndiyo maana nimejikuta tu nikijiuliza, hivi Agnes akiambiwa kuwa anajiuza kupitia mitandao ya kijamii, atakataa?
0 comments:
Post a Comment