Awali, OFM ilipokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo juu ya vijana hao kufanya ngono vichochoroni na kusababisha kuzagaa kwa maboksi ya mipira ya kiume (kondom) maeneo hayo kutokana na kutupwa hovyo baada ya kutumika.
Baada ya kufanya utafiti na kuona hali halisi, OFM wakishirikiana na askari kutoka kituo kidogo cha polisi cha Mbagala-Kizuiani, walitinga katika eneo hilo saa nane usiku hivi karibuni na kuwanasa laivu machangu kadhaa na wateja wao katika banda moja la mama ntilie.
Mbali na eneo hilo, OFM ilishuhudia vibanda vingine vinavyotumiwa na machangu hao na wateja wao kufanya ngono na kujionea kondom na makasha mengi yaliyotumika kwa siku hiyo.
Mwishoni, machangu hao na wateja wao walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kisha mapema siku iliyofuata walipandisha Mahakama ya Jiji la Dar kusomewa mashitaka ya uzembe na uzururaji.
Endapo wakikutwa na hatia hukumu yao ni kifungo cha miezi sita au faini ya shilingi elfu 50 au adhabu zote kwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment