ATUPWA JELA MWAKA MMOJA KWA KOSA LA KUTUMIA JINA LA NAPE NNAUYE KUTAPELI


MAHAKAMA ya Wilaya ya Geita imemhukumu Selemani Nkwenda (36) kwenda jela mwaka mmoja baada ya kumtia hatiani kwa kutapeli watu kwa kutumia jina la Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.
 
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu wa mahakama hiyo, Zablon Kesase, alisema ameridhika pasipo shaka kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
 
Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na makosa mawili na kila kosa atatumikia kifungo cha miezi sita, hivyo atatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

>>Tanzania daima 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini