ATHARI ZA KUHARAKISHA FARAGHA-2

 
WENGI huamini kukutana faragha huzidisha mapenzi katika uhusiano. Inawezekana ni kweli lakini tendo hili huwa na ubora na maana zaidi ikiwa litafanywa na wanandoa.
Kutokana na mabadiliko ya dunia, faragha imekuwa ni jambo la kawaida kabisa hata kwa wale ambao ni marafiki tu. Wanaofanya hivyo, huwa na imani kuwa wanawapagawisha wapenzi wao na kuwafanya wasifikirie kuwaacha.

Tendo la ngono limekuwa jambo la kawaida. Ni jambo ambalo linaweza kusababisha hata uhusiano kuvunjika. Siku hizi marafiki tu nao eti wanadai wana haki na tendo hilo.
Kiukweli ni kwamba tendo hilo hufanyika sana, ndiyo maana mada hii ikawepo ili kuwashtua vijana wajitambue na kushika utaratibu mpya. si vyema kuliacha jambo hili, kwa sababu linafanyika.

Hata hivyo, zipo athari zinazoweza kupatikana ikiwa tendo hilo litaharakishwa (maana lazima litafanyika). Wiki iliyopita nilianisha athari nne, leo tunamalizia mada yetu.
Kwanza nilieleza kwamba hupunguza thamani ya mwanamke, hupunguza msisimko, nikaelezea kuhusu upungufu na mwisho kupoteza msimamo. Sasa tumalizie.

(v) Mimba
Kuna suala la mimba. Nimekutana na kesi nyingi sana za aina hii. Wanaokutana kimwili na wenzi wao bila mpangilio huwa hawazingatii suala la mimba lakini inapotokea ndiyo huanza kuhangaika kutafuta ushauri.

Ndugu zangu, kama hujui hili, ngoja nikuambie, wanawake wengi wawapo faragha na wenzi wao huwa hawana ujasiri wa kuulizia kuhusu kinga.
Wanawake mara nyingi huwa hawanunui kinga wakati wakienda kukutana na wenzi wao. Ni kama vile anasikilizia mwenzi wake anavyotaka. Kama akitaka kutumia sawa, kama akikataa baasi!

Utafiti unaonyesha kuwa, wanawake wengi wanapokuwa faragha, akili na mawazo yao yote huwa katika kuwafurahisha wapenzi wao tu, mambo mengine huyapa nafasi ndogo sana. Hii ndiyo sababu hupata mimba bila kujiandaa. itaendelea wiki ijayo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini