Leo nina tatizo naomba ushauri na msaada kimawazo..
Nimekuwa na mme wangu kwa miaka minne sasa na tumebahatika kupata mtoto ana 2 years old girl
Jmos moja mme wangu alinipa simu yake kuongea na mama mkwe baada ya kumaliza kuongea nikawa najifunza kutumia smart phone ya husb tukiwa kwenye sherehe nilishawishika kuingia kwenye picha
na whatsApp pia
Huko nikaanza kuingia kila sehemu..Ile nafika WhatsApp walahi niliumia oho sana Mme wangu alikuwa anachat na wakina dada tofauti tofauti mambo ya mapenzi na kuombana kutumiana picha ...na mengineyo sipendi kusema
Pia nilikuta kwenye Picture profile mme wangu ana picha zaidi ya sita za kina dada waliomtumia kwenye WhatsApp
Nilimuuliza mme wangu hakunipa maneno ya kueleweka ,na mimeshajua mwenzangu ananicheat wakati mie nimejituliza nyumbani nalea mwanangu wa miaka miwili.
Lakini Bado nimesikia sasa ni kilio cha wanandoa wengi na mahusiano yanavunjika kwa sababu ya hizi wasapu..
Wapenzi niambieni nifanyeje roho inaniuma sana!naichukia ndoa kama ndo kuna usaliti wa hivi
0 comments:
Post a Comment