STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘ Nisha’ anadaiwa kuwa na gundu
kwa wanaume kwani kila akipata mchumba huwa anaporwa ambapo safari hii
amenyang’anywa bwana’ke mpya ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva,
Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, Risasi Mchanganyiko limesheheni.
ISHU YAANZIA BBM
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni mwanadashosti huyo aliamua kujifungia ndani na kushindwa kujitokeza mbele za watu baada ya kuenea kwa habari za kusalitiwa na Ney wa Mitego.
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu na Nisha kilitonya kuwa msanii huyo alianza kujua kuwa hana chake kwa mwanamuziki huyo baada ya jamaa huyo kutundika picha za binti kwenye mtandao wa kijamii wa BBM na kuanza kummwagia sifa kuwa ndiye mtu wake.
“Dah, unaambiwa Nisha alikuwa anapigiwa simu kila dakika hadi akaamua kuizima. Si unajua tena wapambe? Kiukweli Nisha alianza kuwaza sana kuanzia huko nyuma, yaani kila akipata mwanaume anaporwa so (kwa hiyo) anajiona kama ana gundu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Anachotaka Watanzania wajue ni kwamba kwa sasa yupo single (hana mpenzi) kwani mapenzi na Ney wa Mitego yalikwisha zamani.”
Kabla ya Ney wa Mitego, Nisha aliwahi kuwa na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Godfrey Kusila ambaye naye aliporwa na mwanamke aliyeibuka na kudai kuwa jamaa huyo alikuwa mumewe.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilizama kwenye BBM na kujionea namna Ney wa Mitego alivyokuwa akimnadi mrembo wake mpya huku watu wakimsema Nisha kimafumbo.

NISHA ANASEMAJE?
Hata hivyo, alipotafutwa Nisha na kuulizwa juu ya kusalitiwa na Ney wa Mitego, aligoma kufafanua kwa madai kuwa hayupo kwenye ‘mudi’ nzuri ya kulizungumzia suala hilo.

0 comments:
Post a Comment