MWANAFUNZI WA CHUO CHA AFYA BUGANDO AJISHINDIA GARI YA KAMPUNI YA BEFORWARD KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

Bwa.Marco Hingi akifurahia mara baada ya kujishindia gari hilo aina ya Noah kutoka kampuni ya Be Forward  ****
Kampuni ya uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka JAPAN ya BEFORWARD imeendesha shindano la kuwapata washindi 25 duniani kote waliojielezea jinsi wanavyoweza kuitumia kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambapo mtanzania MARCO HINGI ameibuka mshindi na kujishindia gari.

Akizungumza jijini DSM Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA amesema shindano hilo liliendeshwa wakati wa sikukuu ya CHRISMASS ambapo wateja waliotembelea ukurasa wa facebook wa befoward walipata nafasi ya kuulizwa maswali na kujibu mambo kadha wa kadha  

Kati ya washindi hao Tanzania imepata nafasi mbili ambapo mwanafunzi wa chuo cha afya cha BUGANDO MWANZA bwana MARCO HINGI ameibuka mshindi

Makabidhiano ya zawadi ya gari aina ya NOAH yenye thamani ya shilingi milioni 11.8 yamefanyika leo jijini DSM kati ya Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA na Mshindi MARCO HINGI ambapo SHIBATA amesema hiyo ni moja ya mikakati yao ya kuongeza mauzo kwa kuwafanya wateja kuwa na imani nao kama anavyoeleza meneja mkuu ISAAC MBINILE  
 
Kwa upande wake MARCO HINGI ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha  afya BUGANDO mwanza amesema aliwaomba BEFORWARD kumpatia gari la kubebea wagonjwa kutokana na mradi wake alioubuni wa kusaidia mama wajawazito vijijini.

Aidha HINGI ameongeza kuwa baada ya kujibu swali la BEFORWARD walijitokeza watu wengi waliolipenda wazo lake kwa kuandika ‘like’ na hatimaye kuibuka mshindi.HINGI amesema atalitumia gari hilo kubebeea wagonjwa katika mradi huo waliouanzisha mkoani MWANZA

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini