Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na
kumfanya Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.
“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika
sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana
kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Linah kupitia simu yake ya kiganjani ili
kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu
kujitambulisha, staa huyo alikata simu.
“Nani kakwambia kwamba nina mimba? Hayo ni maneno ya watu,
wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,”
alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila
siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.
0 comments:
Post a Comment