MBOWE ALIVYO ZIMA VURUGU BUNGE LA KATIBA, KURA ZARUDIWA KUHESABIWA

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe ameonyesha ukomavu mkubwa katika uongozi na masuala ya siasa baada ya kufanikiwa kumwongoza Mwenyekiti wa Bunge maalum la kumtafuta Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo.
Mwenyekiti wa Bunge hilo Oliva Luena alikubwa na wakati mgumu wa kuliongoza bunge hilo, lenye wajumbe zaidi ya 548,katika mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa muda,hali ilikuwa tete ndani ya ukumbi huo wa bunge baada ya kura kuharibika kutokana wajumbe zaidi 45 kuongezeka, badala ya wajumbe 548 waliokuwepo wakati wa zoezi la kupiga kura.
Hatua hiyo ilimlazimu Mwenyekiti huyo kuamuru zoezi la upigaji kura urudiwe,huku baadhi ya wajumbe wa bunge hilo maalum wakipinga hatua hiyo kwa madai kwamba itapoteza muda na pengine wakaja kurudia tena zoezi hilo.
Wajumbe hao waliokuwa wakizungumza bila kufuata utaratibu, huku wakishindwa kumsikiliza Mwenyekiti wao Luena kutokana na kile walichodai kwamba kura zilizozidi ziondolewe,huku wengine wakidai kwamba kila mjumbe ahesabiwe kwa mtindo wa namba moja hadi mwisho yaani kila mmoja asema namba moja hadi wa mwisho.
Hata hivyo hali hiyo ilimfanya Mbowe asimame na kuzungumza kwa hekma na busara huku akimtaka Mwenyekiti huyo kufuata ushauri wake, ambapo alisema kwamba,  "Mwenyekiti naomba utumie hekma kurudia zoezi la kura kupigwa upya", kauli ambayo ilipingwa na baadhi ya wajumbe.
Mbali na kupingwa vikali na baadhi ya wajumbe waliokuwa ndani ya ukumbi huo wa bunge, huku mjumbe mmoja akizungumza ovyo na kusema kwamba kila mmoja asimame nyuma ya mgombea anayempenda ndipo wahesabiwe.
Wajumbe hao pia hawakuzingatia hata heshma ya kiti aliyokalia mwenyekiti Oliva Luena kuwapa nafasi, Mbowe bado hakutaka kutumia jazba badala yake akaendelea kusisitiza kwa kauli ya upole,hekma na busara kumuomba mwenyekiti huyo kukubali ushauri wake wa kura kudiwa.
Mbowe alisema,"Mwenyekiti mimi nina mambo matatu ya kukushauri katika zoezi hili, moja milango yote ifungwe ili watu wasiokuwepo huku ndani wasiingie kuvuruga uchaguzi huu,pili wajumbe wote wakae chini,tatu karatasi za kupigia kura,zigawiwe kwa kila mjumbe kwa kupelekewa kwenye kiti chache, kwani kwakufanya hivi tutakuwa tumekwepa historia mbaya ya kura kurudiwa ndani ya nchi hii".Hatimaye Mwenyekiti wa bunge la mpito Oliva Luena alikubaliana na ushauri huo na kuamuru zoezi la upigaji kura urudiwe. Wagombea waliokuwa wakipigiwa kura ni pamoja na Pandu Ameir Kificho ,Magdalena Lubangila,Professa Coaster Rick

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini