Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja.
STAA wa
sinema za Kibongo, Kajala Masanja amejikuta katika hali mbaya kufuatia
kunyweshwa sumu na mtu ambaye hakuweza kufahamika mara moja.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita maeneo ya Tegeta jijini Dar katika Klabu ya Seventy One ambayo alikwenda kujiachia na marafiki zake.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita maeneo ya Tegeta jijini Dar katika Klabu ya Seventy One ambayo alikwenda kujiachia na marafiki zake.
“Unajua mambo ya klabu tena, kila mtu alikuwa bize na mambo yake,
hivyo hatukuweza kugundua mara moja kuwa nani alihusika, lakini
tulishangaa ghafla Kajala alijisikia vibaya hivyo marafiki zake wa
karibu walimkimbiza nyumbani kwao kisha hospitali,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya paparazi wetu kuzinyaka habari hizo, Jumanne iliyopita (juzi) alimtafuta Kajala ambaye alikuwa amejipumzisha nyumbani kwa njia ya simu, akaeleza kwa shindashinda jinsi tukio hilo lilivyokuwa:
“Ilikuwa Jumapili usiku, nilikuwa nimekaa na washkaji zangu pale
klabu akiwemo Mubenga, sasa niliagiza juisi pale nikaanza kunywa, funda
la kwanza…la pili nikaanza kujisikia vibaya.
“Nilisikia kama kichefuchefu, nikatoka nje ambapo hali ilizidi kuwa mbaya. Marafiki wakashauri nirudishwe nyumbani, nako hali ikazidi kuwa mbaya.
“Nilisikia kama kichefuchefu, nikatoka nje ambapo hali ilizidi kuwa mbaya. Marafiki wakashauri nirudishwe nyumbani, nako hali ikazidi kuwa mbaya.
“Wakanipeleka hospitali ambapo madaktari waliponipima walinambia
nimekunywa kitu chenye sumu hivyo wakanipa dawa za kuondoa sumu mwilini
na nashukuru Mungu, naendelea vizuri.”
Alipoulizwa kama ana ufahamu wowote juu ya aliyehusika na kama anaweza kumchukulia hatua zozote, Kajala alisema anamuachia Mungu kwani anaendelea vizuri.
“Mimi nashukuru bado napumua, siwezi kujua aliyefanya hivyo alikuwa na dhumuni baya kwangu au iliingia kwa bahati mbaya, naendelea vizuri,” alisema.

0 comments:
Post a Comment