HUYU NDIYE MSANII ALIYEFARIKI JUMANNE HII, ALIKUA KATIKA TAMTHILIA ILIYOKUA IKIONYESHWA ITV..

Pili Ramadhani ‘Awena’ wakati wa uhai wake.
KUNDI la Jakaya Arts Group limepata pigo tena baada ya kumpoteza msanii mwenzao wiki mbili zilizopita ambapo kifo kimemchukua msanii mwingine ambaye ni Pili Ramadhani ‘Awena’ (33) aliyekuwa akiishi Ubungo-Kibangu jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo alifariki Jumanne wiki hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa na uvimbe kwenye utumbo. Uvimbe huo ulisababishwa na upasuaji ambao ulipelekea ujauzito aliokuwanao kuharibika ndipo aliporudishwa tena hospitali kwa ajili ya kusafishwa.
Kwa mujibu wa ndugu wa familia hiyo aliyefahamika kwa jina la Omari, mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda kuzikwa kwao Morogoro.
Awena ameacha watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume. Miongoni mwa muvi alizocheza ni pamoja na ‘Family Mistake’ ambayo iko katika foleni ya kutoka na pia alicheza muvi mpya ya RJ inayoitwa ‘Bad Luck’.





TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini