NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Perreira Ame Silima, amesema uwepo wa fedha chafu nchini umechangia kuendelea kukua kwa uhalifu.
Kwa mujibu wa naibu waziri huyo, matendo hayo ya uhalifu ni
usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara ya binadamu na mitandao ya
kigaidi nchini.
Akifungua mkutano wa siku sita wa wakuu na maofisa wakuu waandamizi
wa Jeshi la Polisi kwenye ukumbi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi
(MPA) alisema kuna ongezeko la makosa makubwa na madogo ikilinganishwa
na vifaa vilivyopo vya kupambana na uhalifu huo.
Alisema kuwepo kwa ukuaji wa uhalifu hasa ule wa kimataifa, hatua
mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo kutunga sheria zinazoharamisha makosa
hayo.
0 comments:
Post a Comment