DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU KUCHAGULIWA KWENDA KUWANIA TUZO MAREKANI



Msanii Diamond kutoka Tanzania ni moja ya wasanii kadhaa kutoka Africa Hasa afrika magharibi watakaoshiriki katika Tuzo za muziki zitakazofanyika huko Eisemann Center Dallas Nchini Marekani



Tuzo hizo zinazotaraji kufanyika July 26th, 2014 na kuwakutanisha wasanii kutoka Africa Magharibi Kusini na Kwinginepo Itahostiwa na mchekeshaji kutoka Nigeria Basket Mouth pamoja na Na Mrembo Pia Muigizaji Kutoka Nollywood Juliet Ibrahim.

Unaambiwa mambo ya Ya Red Carpet yataanza saa moja kamili huku show kamili ikianza saa mbili kamili

Show Hiyo Kubwa kwa wa Africa Itakusanya wadau kibao wa muziki wa kiafrika Duniani Wanamuziki, Ma producer, Ma Manager, Dj’s Na kila anaeendeleza Tamaduni Za Kiafrica

Wageni kutoka Mataifa 17 Ya Africa wanatarajia kutoka Miji ya mbali mbali ya Nchini Marekani kuhudhuria Tuzo Hizo Ambapo kwa hapa Tanzania tunatarajia kuwakiliswa na msanii mkubwa Diamond Platinum.

TAZAMA VIDEO AKIFUNGUKA

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini