CHADEMA WAMVAA RAIS KIKWETE , WAMPA SIKU 3 ZA KUIFUTA KAULI YAKE....NAPE NNAUYE AJIBU MAPIGO, ADAI KUWA RAIS KIKWETE HAWEZI KUIFUTA KAULI HIYO, ASISITIZA KUWA DAWA YA MOTO NI MOTO



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempa siku tatu Rais Jakaya Kikwete awe amefuta kauli yake aliyoitoa Februari 15 mwaka huu, mjini Dodoma baada ya kufunga Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Kauli hiyo ni ile iliyowataka wanachama wa CCM kuacha unyonge badala yake wajibu mapigo ya wapinzani hasa wanaoendesha siasa za vurugu katika kampeni za uchaguzi.

Rais Kikwete aliongeza kuwa, uvumilivu una kikomo kwani ni muda mrefu wana CCM wamekuwa wakifanyiwa vitendo visivyo vya kistaarabu kiasi cha kufikia hatua ya kuumizwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA, Bw. Singo Bensoni, alisema kama Rais Kikwete atashindwa kufuta kauli hiyo, chama hicho kitachukua hatua.

Alisema kauli hiyo ni ya hatari kwa vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla hivyo asipoifuta watalifikisha jambo hilo ngazi za kimataifa kwa hatua zaidi.
 
"Hadi sasa , CHADEMA tunasikitika kuona hadi sasa, Rais Kikwete ameshindwa kutoa tamko juu ya hujuma za CCM dhidi ya wanachama wa CHADEMA katika matukio mbalimbali yanayotokea nchini," alisema Bw. Bensoni.

Alisema chama hicho hakipo tayari kuiacha kauli hiyo iendelee kukaaa vichwani mwa Watanzania bila kufutwa hivyo watahakikisha wanachukua hatua stahiki.
 
Nape ajibu mapigo 
Akijibu  mapigo  hayo; Nape ameitaka CHADEMA kuwa na nidhamu kwa Rais Jakaya Kikwete na kuacha kuweweseka.

Alisema kamwe Rais Kikwete hawezi kufuta kauli yake na kwamba, itakuwa kali zaidi ili kukomesha vitendo vya vurugu vinavyofanywa na wafuasi wa CHADEMA.
“Mwenyekiti wetu hawezi kufuta kauli yake, CHADEMA wametufanyia unyama…tunawasubiri Kalenga waje wafanye hayo mambo yao tena.
“Kama wao ni jeshi la angani basi na sisi ni jeshi la nchi kavu na dawa ya moto ni moto, nina maanisha kuwa kama wao watatumia helkopta kufanya kampeni sisi tutatumia magari,” alisema Nape.
Hata hivyo, Nape alisema mchezo mchafu wa CHADEMA kuanza kuzitumia taasisi zisizo za kiserikali na wanaharakati kutoa matamko hayo umebainika.
“Tayari kuna taasisi ilishatoa taarifa, huu ni mpango endelevu, lakini ni mambo ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini,” alisema mmoja wa viongozi wa Chama hicho makao makuu.
Utekelezaji wa matamko hayo yanafanywa na taasisi moja inayomilikiwa na chama hicho (jina linahifadhiwa), ambapo jana chama hicho pia kilitoa tamko la kumtaka Rais Kikwete aombe ardhi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini