Tanzania bado ipo kwenye mgogoro na nchi
ya Malawi juu ya mpaka halisi wa nchi,Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mh Benard Membe amesema hatma juu ya mgogoro
huo inategemewa kutolewa mwezi march.
Hukumu hiyo itaamuliwa baada ya jopo la Usuluhishi litakapokaa na kusikiliza pande zote mbili ambalo litaongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano
Kupatikana kwa suluhu ya mgogoro wa mpaka huo kutawatoa hofu wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa hilo ambao wamekuwa wakitegemea shughuli za uvuvi wakiwemo wakazi wa kijiji cha Manda Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.
Wakazi wa eneo hilo wamesema kwa hivi karibuni tangu kutulia kwa vuguvugu la mgogoro huo wamekuwa wakiendelea shughuli zao za maendeleo kama kawaida ikiwemo uvuvi.
0 comments:
Post a Comment