HATIMA YA PINGAMIZI LA ZITTO KABWE KUJULIKANA JUMATATU, WAFUASI WA CHADEMA WATWANGANA NGUMI MAHAKAMANI


 
Leo ilikua itoke hukumu ya  kesi iliyopo baina ya Zitto Kabwe na CHADEMA   ambapo kulikuwa  na  mabishano  makali ya kisheria dhidi  ya  pande  zote  mbili . 

Hukumu hiyo haijatolewa  na  badala  yake  mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imeamua kuahirisha kesi hiyo mpaka jumatatu ya tarehe 6 Januari saa 4 asubuhi ambapo hukumu juu ya madai yaliyopo mahakamani itatolewa.

Nje  ya  mahakama  hiyo  hali  haikuwa  nzuri  baada  ya  vurugu  kuibuka  kati  ya  kundi linalounga  mkono  maamuzi  ya  CHADEMA   na  lile  linalomuunga  mkono  Zitto  Kabwe..

Makundi  hayo  yalijikuta  yakitwangana  ngumi   mahakamani, hali  iliyowafanya  polisi  waingilie  kati. 
 
 
 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini