SERIKALI YA ZANZIBAR YAKABIDHI NYUMBA MPYA KWA WANANCHI WAKE IKIWA NI MOJA YA SERA ZAKE ZA KUWAJENGEA WANANCHI WAKE MAKAZI MAZURI


Rais mstaafu  wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume amesema majumba ya Mpapa yaliyokabidhiwa kwa wananchi 24 kutoka shehia 6 ya jimbo la bambi  yanahitaji kulindwa na kutunzwa ili yaweze kudumu zaidi uhai wake.

Hayo ameyasema huko bambi wakati alipokua akiyakabidhi nyumba hizo kwa familia kadhaa katika sherehe za kuzifungua nyumba hizo kwa wakazi waliopewa,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanbar.

Amesema azma ya awali ya mapinduzi ya Zanzibar ni kumpatia makazi bora mwananchi wa Zanzibar  na hiyo ndio iliokuwa azma ya Rais wa awamu ya kwaza,Hayati Abeid  Aman Karume ya kuwajengea wananchi wake makazi hayo,hivyo azma hiyo ipo palepale na serikali haitorudi nyuma.

Amesema ujenzi wa nyumba hizo,umemalizika na kuazia leo ni huru kwa wananchi kuzitumia kwa kuweka familia zao. Sambamba na kuyatunza kwa ubora.

Nae Waziri wa Ardhi,Maji,Ujenzi na Nishati wa Zanzibar,Mh. Ramadhani Abdalla Shaban amesema wameshapitisha maamuzi ya kuazisha Shirika la Nyumba ambalo litasimamia ujenzi na ukarabati wa nyumba zote na maendeleo yake kwa kushirikiana na wakazi wanao ishi kwenye nyumba hizo.

Aidha akijibu maombi ya wana kijiji wa Mpapa kuhusiana na tatizo la maji katika nyumba hizo,amesema zitapatiwa maji si muda mrefu,tatizo la maji Mpapa litakuwa historia kwa kushirikiana na Mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini