Mwanafunzi wa kike,13, (jina linahifadhiwa) anayesoma
darasa la tano katika shule ya Msingi Unyakumi, mkoani Singida,
amefanyiwa unyama kwa kubakwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la
Mapunda ambaye ni dereva wa bodaboda.
Akizungumza kwa shida kutokana na maumivu makali aliyonayo akiwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, denti huyo alisema kwamba mkasa
huo ulimpata Novemba 19, mwaka huu wakati akitoka shule akielekea
nyumbami kwao.
Akisimulia mkasa huo mwanafunzi huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi ni mtoto yatima wa kufiwa na baba, mama naye aliachana na baba
nikiwa na umri mdogo, nimekulia katika shida tena kwa kulelewa na watu
tofautitofauti, niliona kitakachonikomboa ni elimu lakini ndoto yangu
sasa imekufa.
“Imekufa kwa kuwa nateseka kitandani kwa muda mrefu sasa kutokana na
maumivu yaliyotokana na kubakwa.Nimekua wa kujisaidia kitandani,
nawakumbuka wazazi wangu, leo hii wangekuwepo wangekua watetezi wagu,
sina uhakika kama nitapona na kwenda shule tena.
“Kutoka
shuleni hadi nyumbani ni mwendo wa saa moja, siku hiyo niliyobakwa
ilikua Ijumaa, nilikua natoka shule nikielekea nyumbani, njiani kuna
vichaka na mashamba ya mikorosho, nilipofika karibu na banda bovu
nilimkuta kijana amekaa juu ya jiwe.
“Nilijisikia vizuri sana nilipomuona, uoga ulinitoka juu ya wanyama
wakali, sikua na hofu ya aina yoyote kama angenigeuka, nilipomkaribia
alinikamata kwa nguvu, alinivuta akanipeleka katika banda bovu.
“Nilijaribu kujinasua lakini nilishindwa kwani alikua na nguvu kuliko
mimi, niliamua kupiga kelele ili nipate msaada toka kwa mtu yeyote
anayepita, hata hivyo, hakuna aliyejitokeza, alinifunika mdomo,
alinipiga, niliishiwa nguvu, akaniingilia, alipomaliza haja yake,
akakimbilia pasipojulikana.
“Nilitokwa damu nyingi zilizotoka sehemu za siri, niliinuka na
kutembea kwa shida kwani hata kiuno kilikua kikiuma sana, nilifika
nyumbani, sikumkuta dada kwani alikuwa ana kawaida ya kurudi usiku
akitokea kazini kwake.
“Aliporudi alikuta nimeshafua nguo zangu na nimeshalala, niliona aibu
kumweleza, ilipofika Jumapili maumivu ya kiuno na sehemu za siri
yakaongezeka, nilikua nikitembea kwa shida, ilimbidi dada aniulize nina
nini? Awali niliogopa kumweleza lakini baadaye nilimsimulia kila kitu
kwani maumivu yalizidi.
“Nilishindwa hata kwenda shule, nilipelekwa hosptali ya wilaya lakini
hali yangu ilizidi kuwa mbaya. Nikahamishiwa hospitali ya mkoa, Singida
lakini sikuweza kupata nafuu, nikaletwa hapa Muhimbili kwa gari la
wagonjwa ‘ambulance’ kwani nilishindwa kukaa kwenye kiti cha basi.
“Bado sijaweza kukaa wala kuinuka, hata kulala kwangu ni kifudifudi,
nalishwa, naogeshwa kitandani, kwa kweli sina raha hata kidogo tangu
nifanyiwe unyama huo maana sijaenda shule, wenzangu wamefanya mitihani
mie sipo, nauguza mamivu.
“Nimeoza sehemu za siri hadi makalio, natokwa na usaha, siamini kama
nitapona na kwenda shule tena. Aliyenitenda haya tunaishi naye mtaa
mmoja na hajawahi kunitongoza ila aliamua kunibaka.
“Nimefikishwa hapa Muhimbili Novemba 20, mwaka huu, naomba taarifa
hizi zimfikie mama popote alipo kwani aliachana na baba akarudi kwao
Musoma,”alieleza kwa uchungu denti huyo.
Dada wa mtoto huyo anayeishi naye aliyejitambua kwa jina moja la Rose
alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri kutokea na ameiomba serikali
imkamate mtuhumiwa ili haki itendeke.
Source: Global Publisher.
0 comments:
Post a Comment