WEMA SEPETU NA DIAMOND WANASWA WAKINYONYANA DENDA HADHARANI

Nasibu Abdul ‘Diamond’, na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi la mahaba
MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, walijikuta wakionesha upendo wao mbele za watu kwa kudendeka  barabarani, Amani lilishuhudia.
Ishu hiyo ambayo wapendanao wengi huifanya kwa faragha, ilijiri hivi karibuni maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo ni hatua chache kutoka kwenye Ofisi za Global Publishers ambao ni wachapishaji wa Magazeti Pendwa ya Amani, Risasi, Uwazi, Ijumaa, Championi na Ijumaa Wikienda.

ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, Wema alikuwa kwenye shughuli zake za kila siku maeneo hayo ambapo alikuwa ameegesha pembeni gari lake la rangi ya pinki aina ya Toyota Lexus Harrier bila kujulikana alikokuwa ameelekea.

Wakionyeshana upendo hadharani
DIAMOND AIBUKA PEKE YAKE
Ikadaiwa kuwa, mara Diamond naye alitokea bila kujulikana alikotokea akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Prado na kuegesha gari lake jirani na alipoegesha Wema.


SIMU YAPIGWA CHUMBA CHA HABARI GLOBAL
Mapaparazi wa Global wakiwa katika kazi za kila siku ndani ya ofisi, simu ilipigwa kwa mmoja wao na kutonywa kuhusu wawili hao kuwepo eneo hilo kimahabamahaba.

“Jamani Global hapa jirani na ofisi zenu Diamond amekuja sasa hivi, lakini inaonekana amemfuata Wema maana Wema alishakuwepo muda mrefu uliopita, njooni mchukue picha si ndiyo zenu au bado mna bifu na Wema tangu siku ile alipokuja kuwafanyia fujo?”

PAPARAZI AWAFIKIA
Haraka sana paparazi mmoja alibeba kamera yenye uwezo wa kupiga picha kwa umbali wa mita hata 250 bila mhusika kushtukia na kutoka nayo.

Kweli, lilikuwa tukio lilionesha kushangaza kwani paparazi alikuta wapita njia wakiwa wanapunguza mwendo ili kuwashuhudia wawili hao walichokuwa wakikusudia kukifanya bila kuogopa watu.
WEMA NJE, DIAMOND NDANI
Kamera ya paparazi wetu iliweza kuwanasa wawili hao, Wema yeye alisimama nje ya gari la Diamond upande wa dirisha la dereva na kuongea na mwandani wake huyo jambo ambalo hakuna mpita njia aliyeonekana kushangaa.
Hata hivyo, mshangao ulianza pale Diamond alipotoa mkono nje na kumshika kiuno Wema huku wakiendelea kuongea ndipo baadhi ya wapita njia nao walipokoleza macho kodo, wengine wakihoji kama aliyesimama nje ya gari ni Wema, nani alikuwa ndani ya gari hilo!

Haikuwa rahisi kupata majibu kwani wengi walikuwa wanashindwa kumwona Diamond. Wengine waliamini kwamba, Wema alikuwa ameshikwa kiuno na mwanaume mwingine ambaye huena akampindua Diamond kama na yeye alivyompindua yule kigogo wa ikulu ‘CK’.
“Sasa mbona Wema anakubali kushikwa kiuno hivihivi tu, haoni watu?” alihoji mpita njia mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Salome, mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar.

DENDA NJE NJE
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kushikwa kiuno, Wema alikwenda mbali zaidi pale alipomwinamia ‘baby’ wake huyo na kula naye denda ambapo naye mwanaume hakufanya ajizi hata kidogo.

“He! Jamani! Naona wenzetu leo wameamua, hata barabarani? Huu ustaa nahisi unawafanya watu wawe vichaa mbele za watu. Mimi siwezi kabisa kudendeka mbele za watu,” alisema mrembo mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake lakini naye ni denti wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ambacho kipo jirani kabisa na eneo la tukio.

DIAMOND ACHOMOKA KWA KASI
Baada ya denda hilo lililodumu kwa dakika moja, Diamond alimuaga Wema na kukanyaga mafuta kuondoka katika eneo hilo huku wananachi wakimfuatilia kwa macho yaliyojaa mshangao.

Soma Habari Kamili

JACQUELINE WOLPER: NATAKA SERIKALI 2

Muigizaji staa Bongo, Jacqueline Wolper
MWIGIZAJI staa Bongo, Jacqueline Wolper ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema yeye matakwa yake ni kuwepo kwa serikali mbili na si tatu wala ya mkataba.
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar, Wolper alisema anaamini serikali ya tatu itakuwa mzigo kwa wananchi ambao ndiyo walipa kodi.

“Serikali mbili ndiyo mpango mzima, ya tatu ni mzigo, ya mkataba sioni maana yake. Halafu nataka muungano udumu, pia nitafurahi sana kama Ukawa watarudi bungeni litakapoanza tena Agosti mwaka huu,” alisema Wolper.

Soma Habari Kamili

MAINDA AACHANA NA UIGIZAJI WA FILAMU ZA KIBONGO, AMRUDIA MUNGU NA KUANZA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI!

Msanii wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’
MSANII wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’  aliyewahi kutamba na filamu za kidunia, sasa ameamua kuimba muziki wa Injili ikiwa ni kumtukuza Mungu na kujiandalia maisha mema ya peponi.
Akipiga stori na mwandishi wetu juzi, staa huyo aliyekuwa akiitwa Mwanaidi na kubadili jina baada ya kuokoka, alisema: Vijana siku zote tuna nguvu, tuna muda wa kutosha hivyo tunapaswa kumtumikia Mungu siyo mpaka tuchoke, tuzeeke au tufanye kwanza dhambi ikifika omega (mwisho) ndiyo unamkumbuka Mungu.
Mainda akiwa kwenye pozi
“Ninaimba kwaya tena sauti ya tatu, subirini muone ujio wangu mpya kwani nimeamua kumtukuza Mungu aliyeumba mbingu na nchi.”

Soma Habari Kamili

NAY AJIBU TUHUMA ZA KUTISHIA KUUA

Staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
STAA wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefungukia skendo ya kumtishia kumuua mdogo wake aitwaye Amani Shija.
Akizungumza na gazeti hili Aprili 29 mwaka huu, Nay alisema kwamba anasikitishwa sana na malalamiko ya Amani kwani katika maisha yake hajawahi kumtishia mtu kumuua na hajui ni kipi ambacho kimemvuta hadi kuanza kulalama mambo kama hayo.
“Hakuna ishu kama hiyo, kwanza Amani siyo ndugu yangu wa damu ila udugu wangu naye niliutengeneza baada ya kukutana naye Ubungo miaka minne iliyopita na akaniomba nimsaidie, bila kinyongo nilianza kuishi naye hadi leo hii anaanza kunitolea maneno kama hayo,” alifafanua Nay na kuongeza:
‘Nay wa Mitego’ akiwa stejini
“Ameshindwa kujielewa lakini mimi namuachia Mungu maana kama kumsaidia nimeshamsaidia sana, nshamlipia hadi chumba zaidi ya miaka minne na nikamtimizia mahitaji yake yote, lakini wapi.” 
Mapema wiki hii, Amani aliripotiwa katika gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa amemfungulia mashtaka polisi Nay wa Mitego kwa madai ametishiwa maisha.

Soma Habari Kamili

JB AANZISHA FUJO NDANI YA KLABU

BIG brother wa filamu za Bongo, Jacob Steven ‘JB’
BIG brother wa filamu za Bongo, Jacob Steven ‘JB’ amezua utata kwenye klabu mpya ya Princess Cassino iliyopo Posta mpya, Dar kufuatia minong’ono kuwa, yeye ndiye mmiliki wake.
Hali hiyo ilijitokeza juzi kati kwenye uzinduzi wa klabu hiyo ambapo msanii huyo ndiye alionekana kuwa mwenyeji kwa kukatiza kila mahali.

“Hivi, JB ndiye mwenye hii klabu nini? Mbona kama mwenyeji kuliko wengine. Anakaribisha wateja, anafuatilia watu kama wanapata huduma sahihi,” alisikika mteja mmoja.
JB alilpoulizwa juzi alikiri kuwa mmoja wa waratibu wa mambo ya burudani ya Cassino hiyo lakini si mmiliki.

Soma Habari Kamili

MLELA ATUPIWA DONGO KUWA TEJA

Nyota wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela
NYOTA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kugeuka teja (mbwia madawa ya kulevya) hali inayomsababishia ashindwe kujichanganya na wasanii wenzake katika shughuli mbalimbali.
Kikizungumza na Amani juzikati, chanzo  kilisema msanii huyo kwa sasa anavuta unga kiasi cha uteja kujionesha waziwazi na kupoteza mwonekano wake wa zamani.
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Mlela na kufanikiwa kumpata nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Katika maisha yangu sijawahi kutumia madawa ya kulevya na huwa nayapinga sana. Wanaosema navuta ni waongo, mimi sasa hivi naitwa baba, hivyo majukumu yameongezeka ndiyo maana sijichanganyi kivile.”

Soma Habari Kamili

GARI LA MZEE GURUMO LAZUA UTATA



Mzee Gurumo akikabidhiwa ufunguo wa gari na Diamond.
AMA kweli asiyekuwepo na lake halipo! Lile gari la aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyefariki dunia hivi karibuni, Muhidin ‘Maalim’ Gurumo alilopewa na nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeibua utata mtupu ndani ya familia ya marehemu huyo baada ya kubainika kwamba kumbe hakupewa kadi yake.
Gari aina ya Toyota FunCargo iliyosababisha hali ya sintofahamu kwenye familia ya mzee Gurumo baada ya kufa.
Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka ndani ya familia hiyo jambo hilo lilifahamika kufuatia mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta miongoni mwa wanandugu hao ambao sasa wamechangukana kutokana na mgawanyo wa mali za marehemu.
Ilijulikanaje kama hakuna kadi?
Chanzo hicho kilimtaja mtoto wa kike wa marehemu Gurumo aitwaye Mariam ambaye anataka nyumba na gari hilo aina ya Toyota FunCargo viuzwe ili watoto wagawane fedha.

Mke wa marehemu mzee Gurumo Pili Said
“Yule binti alikwenda nyumbani kwa mama yake (mke wa mwisho wa mzee Gurumo aliyekuwa akiishi naye kwenye nyumba yake Mabibo, Dar) na kumtaka ampe kadi ya gari akidai ni la kwake na anataka kuliuza.
“Mama mtu alimwambia mwanaye kuwa baba yao hakupewa kadi hiyo siku alipokabidhiwa gari hilo.

“Hata hivyo, mama huyo alisema siku moja mzee Gurumo alimfuata Diamond alipokuwa akifanya shoo pale Coco Beach (Dar) kwa ajili ya kuulizia kadi hiyo ndipo Diamond akamwambia kwamba akitaka kadi amuulize mtu mmoja aliyesema ni kiongozi mmoja, anafanya kazi maeneo ya Posta Mpya jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa),” kilisema chanzo.
Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya Gurumo kuambiwa maneno hayo, hakutoa jibu lolote kwa mke wake kama alipewa kadi hiyo au la, lakini mama huyo hakuwahi kuiona.
Kukosekana kwa kadi hiyo kumesababisha kuendelea kuwepo kwa gari hilo, kwani kama ingekuwepo, lingeshauzwa.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Diamond zilisema kuwa tukio la kutoa gari kwa mkongwe huyo mwanzilishi wa Bendi za  Mlimani Park Orchestra na Msondo Music Band ulikuwa ni mpango maalum wa kumpromoti msanii huyo ili aweze kung’ara zaidi katika vyombo vya habari ambao uliratibiwa na kiongozi huyo mwenye kulalamikiwa na wasanii mara kwa mara.

Diamond ambaye alipongezwa na wadau mbalimbali kwa kitendo chake hicho kilichoelezwa kuwa cha kiungwana na chenye kupaswa kuigwa, juzi hakupokea simu ya mwandishi alipopigiwa ili kutoa ufafanuzi, kama ambavyo hakujibu ujumbe mfupi (sms) aliyoulizwa kuhusu utata huo.
Hata kiongozi huyo alipopigiwa simu, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, pia hakujibu.
Mwaka jana Diamond alimpatia mzee Gurumo gari hilo kama sehemu ya kuenzi mchango wake katika muziki wa Tanzania tukio lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar kabla ya mzee huyo kufariki dunia Aprili 13, mwaka huu.

Soma Habari Kamili

MIPAKA YA HAUSIGELI NDANI YA NYUMBA!-3


Ni matumaini yangu kwamba umzima na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku kama kawaida. Mimi niko poa, namshukuru Mungu kwa kunifanya kuwa miongoni mwa wale wanaoendelea kupumua hadi leo.
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia mada hii. Leo nitaenda moja kwa moja kwenye ile mipaka ya hausigeli ndani ya nyumba nikiamini mwisho wa siku wanandoa watajifunza kitu kitakachoziboresha ndoa zao.
Yapo mambo mengi sana ambayo hausigeli hapaswi kuyafanya ili kuilinda ndoa lakini baadhi ya wanawake aidha kwa kudharau au kutojua wamekuwa wakiyapotezea, matokeo yake unaweza kuingia ndani ya nyumba na kushindwa kujua hausigeli ni nani na mke ni nani.
Hapo ndipo unaweza kusikia habari za hausigeli kutembea na baba mwenye nyumba.
Kuepukana na matatizo hayo, ifuatayo ni mipaka ya hausigeli ndani ya nyumba.
Kwanza; Asiguse kabisa mlango wa kuingia chumbani kwa mabosi wake. Hapa nazungumzia suala la kutoingia chumbani kama ambapo baadhi wamekuwa wakiwaruhusu mahausigeli kuingia na kufanya usafi, jambo ambalo kimaadili halikubaliki.

Msichana wa kazi afanye usafi kote lakini chumbani asiruhusiwe kwani kule kuna siri ambazo hatakiwi kuzijua. Wanaolegeza kamba katika hili ndiyo ambao wanaishia kuvuna mabua.
Pili; Hausigeli asiwe na mawasiliano ya karibu na baba mwenye nyumba. Sasa hivi zipo simu za mkononi ambazo zinatumika katika kurahisisha mawasiliano lakini hausigeli hata siku moja asipewe mwanya wa kumpigia simu baba mwenye nyumba au kumtumia sms.
Baadhi wamekuwa wakiona si jambo baya, matokeo yake inapotokea msichana wa kazi ni mcharuko na baba mwenye nyumba naye hajatulia, wawili hao wanaweza kufungua ukurasa wa dhambi.
Tatu; Hausigeli asihusike katika suala la kufua nguo za ndani za mume. Hapa namaanisha soksi, boksa, ‘singland’ na nyinginezo. Jukumu hili libaki kuwa la mke!
Nne; Hausigeli asiruhusiwe kukaa sebuleni kama baba mwenye nyumba yupo. Wapo ambao wanajifanya wanaishi kizungu, baba yupo lakini na hausigeli naye ameganda sebuleni eti anaangalia tamthiliya, hii siyo sawa kabisa hasa kinidhamu.
Tano; Wakati hausigeli anakwenda bafuni kuoga, kwanza asiwe amevaa nguo nyepesi kama vile kanga moja na pia ahakikishe haonani na baba mwenye nyumba.
Sita; Hausigeli asipewe nafasi kumuandalia kitu chochote mume, kwa mfano chakula, maji ya kuoga, nguo za kuvaa na vinginevyo. Hii ni kazi ya mke lakini utashangaa baadhi yao wamekuwa wakibweteka na matokeo yake wanajikuta wameporwa waume zao.
Saba; Kama baba anakwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani ya mwezi au wiki, asiongozane na hausigeli na kama kuna ulazima, hausigeli aende lakini asikae siti ya mbele.
Nane; Kama familia ina gari, hausigeli asipande akiwa na mtoto mdogo kwenda bichi, kanisani au ‘shopping’ bila kuwepo mama. Hii ni kwa sababu inakuwa rahisi mume ambaye hajatulia kumtongoza hausigeli na mtoto asijue kitu.
Akipanda na mtoto mkubwa mwenye akili ya kutambua mambo haina shida kwani wengi wao huwa wafichuaji wa siri hivyo baba ni vigumu kuongea upuuzi wowote kwa hausigeli.
Tisa; Hausigeli hata kama ana shida vipi, asipewe nafasi ya kumweleza shida zake baba mwenye nyumba. Hata mshahara inashauriwa kuwa mama mwenye nyumba ndiye wa kumkabidhi na si vinginevyo.
 Katika hili pia mke ahakikishe hakuna mwanya wa baba mwenye nyumba kumnunulia vijizawadi msichana wa kazi kwani madhara yake ni kuingia kwenye mapenzi.
Kumi; Hausigeli asimzoee baba mwenye nyumba kiasi cha kuona ni sawa kuzungumza naye wakati wowote na kutaniana kunakostahili kufanywa na wapenzi.
Hayo ni baadhi ya mambo machache ambayo ni vyema yakatiliwa maanani ili kuweza kuzitunza ndoa zetu na kupunguza uwezekano wa baadhi ya mahausigeli kuzipindua.

Soma Habari Kamili

MPENZI WANGU ANANITISHIA KUNILOGA

Huyu alikuwa mchumba wangu ambaye nilimpenda sana na tulikubaliana kuoana. Nilipatwa na matatizo njiani mwenzangu akanambia anaolewa na mtu mwingine (tulikuwa tunaishi mikoa tofauti). Niliumia sana na kutokana na hasira nikamwambia `Tutaona kama utaishi na huyo mwanaume.' Toka hapo sijawahi kuwasiliana naye tena!

Siku za karibuni alinitumia message kwamba anaomba kuongea na mimi, nikamtajia muda ambao ntakuwa free.
Muda huo akanipigia simu na kuanza kunilaumu `@nyalotsi kwanini umenifanyia hivi?'
Nikamuuliza, nimfenyaje?(huku nikiwa na mshangao)
`Umeniroga kila nikipata mimba inatoka, tafadhali sana nisamehe kama nilikukosea! Familia yangu itavurugika.'

Nilikata simu na kuanza kutafakari mambo mengi sana. Ina maana huyu dada kaniona mi mchawi? Mbona hata mizizi ya dawa za kawaida tu siifahamu? Hii laana gani tena? Baadaye nikakumbuka niliwahi kumtishia kwamba hataishi kwa amani na mumewe. Nikampigia simu na kumhakikishia kwamba siwezi kufanya kitu hiyo na wala sio muumini wa mambo hayo.
Nikamshauri pia waende na mumewe hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na wataalamu.!

Kweli duniani kuna mambo!!

Soma Habari Kamili

HIZI NDIO DALILI ZA MAPENZI KUVUNJIKA

Mapenzi ya siku hizi yamebadilika sana tofauti na zamani ambapo siku izi kupotezeana kuko njenje tu wala hakuhitaji gharama yoyote ile,hivyo napenda kushea na nyinyi ni dalili zipi hujitokeza kwa mwanamke na mwanaume wakati mapenzi yanapotaka kuvunjika?

Soma Habari Kamili

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini