

Kuna makabila na tamaduni nyingi nchini Indonesia, lakini
hii ni tamaduni ya kipekee, ya kushangaza na kuogopesha. Tamaduni hii
hujulikana kama sherehe ya kufufua wafu na kuwapeleka kwenye makazi yao
ya kudumu.
Watu wa Toraja, Indonesia huamini kuwa mtu anapokufa huanza
safari ndefu kuelekea kwenye hatima yake, hivyo kuna vitu ambavyo
lazima vifanyike kumsaidia kwenda na kufika salama, ambavyo huhusisha
gharama kubwa. Kutokana na gharama kubwa za mazishi hayo, jamii nyingi
hulazimika kuzika wafu wao katika majeneza ya muda, mpaka baada ya zoezi
la kukusanya pesa kwa aliji ya shughuli ya mazishi kukamilika.
Kwakua ardhi kubwa ya maeneo ya Toraja ni milima, na hivyo
kufanya zoezi la kuwabeba wafu hao kuwa gumu, jamii huamini kuwa wafu
hao huweza kwenda wenyewe kwa kutembea kwa miguu wakisindikizwa na ndugu
zao. Baada ya kufika kwenye makazi yao, inasadikika kuwa wanakufa tena,
ndugu zao huwaosha na kuwavalisha nguo mpya na kisha kuwazika tena.
Kwa siku za hivi karibuni, tamaduni hii imeanza kupotea kwa wakazi
wengi, japo kwa watu wachache wanaoaminiwa na wazee wao kwamba wanaweza
kurithi tamaduni hii, bado wanaifanya
0 comments:
Post a Comment